NASSOR WAZAMBI - MRATIBU "MUNDE STAR SEARCH" |
MUNDE STAR SEARCH
Ni mashindano ya vipaji mbalimbali
ambayo yamelenga kutaka kuwapata na kuibua vipaji mbalimbali
vilivyosahaulika ili kuwakwamua vijana wa chini ya miaka 20 na hata
kutoa fursa za kupata mabalozi watakao kuwa wakiutambulisha mkoa wa
Tabora kwa nyanja nyingi kitaifa, shindano hili limelenga maeneo ya
michezo na vipaji mbalimbali kama KARETI, KICK BOXING, BOXING, UIMBAJI
MUZIKI NA VIPAJI VYA KU-DANCE (Shakes)
Nassor akizungumza na mtandao huu amesema,
"Kilele cha mashindano hayo ni tarehe 28-09-2013 kwa vijana wenye umri wa miaka 20 katika
- UIMBAJI MUZIKI, mshindi atarekodi nyimbo moja pia kupelekwa jumba la vipaji THT (Tanzania House of Talents) na vifuta jasho vitatolewa kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu pamoja na kurekodi katika studio za kawaida.
- KARETI, Mashindano matatu ya kumsaka bingwa wa kareti Tabora.
- BOXING, Mashindano haya yatafanywa ili kuutangaza mchezo huu na kuwaalika mapromota wa mashindano haya ya boxing ili wapate mikataba ili kushiriki miche hiyo kwa faida zaidi ndani na nje ya Tabora.
- KICK BOXING, Hapa pambano moja litahusishwa ili kumpata mshindi wa mchezo huu.
- DANCING (SHAKERING), Hapo mchuano utahusisha vikundi mbalimbali na kushindanishawa kupata kundi moja litakalo nyakua ushindi huo.
UPATIKANAJI WA FORM ZA USHIRIKI:"Form zitaanza kutolewa Jumatano ya tarehe 14-21/08/2013 katika dojo zote za kareti na vituo jimu, maeneo yote wapatikanayo vijana, pia katika kata kupitia madiwani wao NA HAKUTAKUWA NA GHARAMA YEYOTE KWANI LENGO NI KUIBUA, KUINUA NA KUENDELEZA VIPAJI VYA VIJANA WA TABORA" Alisema Nassoro, mratibu wa shindano la MUNDE STAR SEARCH.
ZAWADI NONO ZAIDI YA MILIONI MBILI NA NUSU ZITASHINDANIWA MIONGONI MWA MICHEZO YOTE KWA VIJANA WATAKAO SHIRIKI.