Pages

Ads 468x60px

Featured Posts

Monday, September 15, 2014

PICHA 30 ZA SHOW YA FIESTA TABORA NI SHIDERRRRRR...DUDUBAYA AFANYA SUPRISEE........

Msanii wa muziki wa kizaz kipya ambaye kwa sasa yuko chini ya kampuni ya No Fake Zone,Linah Sanga akiwa jukwaani sambamba na sahabiki wake wakicheza kwa pamoja ndani ya tamasha la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye kwa sasa yuko chini ya kampuni ya No Fake Zone,Linah Sanga akiwa jukwaani sambamba na madansa wake wakilishambulia jukwaa la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora
Msanii mwingine anaekuja vyema kwenye anga ya muziki wa Bongofleva aitwaye Kadja ambaye anatamba na wimbo wake wa Maumivu niache akiimba pamoja na Linah
Wasanii chipukizi kutoka Tabora nao walionesha umahiri wao jukwaani
Sehemu ya umati mkubwa wa watu waliofika kulishuhudia tamasha la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora

Saturday, May 10, 2014

MISS TABORA ALIVYOTWAA MATAJI MAWILI SIKU YA SHINDANO; HIKI NI KIPAJI ALICHOONESHA





Miss Zenna Motte, Mwafunzi wa chuo kikuu cha Mt. Agustino cha Tabora chuo kishiriki cha SAUT anayesomea kozi ya Mahusiano wa Umma na Masoko mwaka wa pili, mshindi wa shindano la Redds lililofanyika wiki jana tarehe 2 mei 2014, hapa alikuwa jukwaani na vazi lake la ubunifu lenye nakshi na mchanganyo wa rangi za bendera ya Tanzania


Miss Zenna Motte, REDDS MISS TABORA 2014. MAY 2
Zenna Motte, hapa alikuwa katika jukwaa akionesha kipaji ambacho kilimpa ushidi wa taji la kipaji hicho kilichotengenezwa kwa muundo wa katuni au mtu ndani ya mtu au waweza sema mtu juu ya kijitu...

Ni nouma sana
Waweza ufe ukicheka.

Warembo walipotembelea redio ya CG FM 89.5 moja ya wadhamini wa shindano hilo (Kushoto ni Zenna na kulia ni Elizabeth ambaye alinyakua taji la mshindi wa pili wa shindano la REDDS MISS TABORA 2014)

Warembo walipata kufurahi katika moja ya klabu ya muziki iliyopo mkoani Tabora wakiwa chini ya usimamizi wa kamati ya maandalizi ya shindano hilo, pia warembo walipokelewa vizuri na uongozi wa klabu hiyo ya One Zero One (101)
Miss Zenna Motte Kushoto akishangiliwa wakati wa utambulisho kama walivyoshangiliwa washiriki wengine.
Hupenda kuwa na watu na watu hupenda kuwa naye pia, mrefu kupita wote na shingo kama ya twiga ni Zenna.... Halaaaaaaaaa....! [PICHA NA aloyson.com]

Wednesday, May 7, 2014

ZENNA MOTTE ndiye MISS TABORA 2014



TBR REDDS 1 TBR REDDS 4 TBR REDDS 7 TBR REDDS 18 TBR REDDS
Washindi wa Mashindano ya Redds Miss Tabora 2014 katikati ni Zena Motte mbaye ndiye mshindi wa kwanza,wapili ni Elizabeth Mkende wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Lencer Kotato kati ya washiriki wanane walioshiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Teofilo Kisanji mjini Tabora.

Friday, May 2, 2014

WARIMBWENDE WATAKAOCHUANA LEO HII "REDDS MISS TABORA 2014"




Bila kukosa show hii itakayofanyika tarehe 02 may, 2014 ndani ya ukumbi wa Teofilo Kisanji kuanzia saa 2 usiku kwa kiingilio cha sh 10,000/= kawaida na 20,000/= kwa V.I.P huku burudani za kutosha kutoka kwa warembo wenyewe na kalizwa na wasanii akiwemo Amini wa "November or December" na nyinginezo, Nemo wa "My Number One" SirMoe wa Freemason na nyingineza kama huu mwaka, knok out n.k.
** USIKOSE **
MISS PAULINE
MISS ELIZA
MISS MWASY
MISS ZENNA
MISS LENCER
MISS SALOME
Mwl wa warembo, (Miss Sarah mshindi wa shindano hili la Redds 2012)
MISS LILIAN
MISS FATUMA
[Picha na aloyson.com]

Tuesday, April 29, 2014

FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI‏

 Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi

Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.

Monday, April 21, 2014

NAY WA MITEGO ALA UJANA NA WANYAMWEZI USIKU WA PASAKA JIONEE HAPA

Nay wa Mitego a.k.a True Boy, nguli wa mziki hivi sasa hapa Tanzania mwenye miondoko ya HipHop, usiku wa Pasaka alitimiza ndoto ya wengi waliokuwa na hamu ya kumuona akila ujana sawasawa katika himaya ya wanyamwezi mjini Tabora.. Amezidi kudhihirisha umahiri wake kwa vibao vikali kabisa kama "salamu zao" Muziki gani" "Nakula Ujana" ambavyo viliwapagawisha mashabiki waliojitokeza katika show hiyo.


Stone wa Kitaa, wakiwakilisha vyema "The Apex" kundi la muziki la mkoani

Picha zote na aloyson.com

Monday, February 17, 2014

HIVI NDIO JINSI SHILOLE, MADEE, QUEEN DARLEEN WALIVYOWADATISHA WANA IGUNGA VALENTINE'S, ANGALIA HAPA


Shilole na Madee wakiwadatisha wakazi wa Igunga kabla ya shoo ya Valentine's Day.
Shilole (kushoto) na Queen Darleen (kulia) wakisema na wana Igunga.
Shilole, wacheza shoo wake na Queen Darleen wakizidi kuwapa raha mashabiki kabla ya shoo yao usiku wa Wapendanao.
Wasanii Zuwena Mohamed 'Shilole' au Shishi Baby, Hamadi Ally 'Madee' na Queen Darleen waliwadatisha vilivyo wakazi wa Igunga mjini siku ya Wapendanao 'Valentine's Day' kabla ya shoo yao iliyofanyika Ukumbi wa Sakao uliopo Igunga Mjin